Swali: Tulisafiri kwenda hajj na pindi tulipopanda ´Arafah gari ikaharibika mwishoni mwa ´Arafah. Baada ya kumaliza kuswali Maghrib tukatengeneza gari na kuendelea na safari. Lakini hata hivyo hatukujua njia. Tukapotea na baadaye gari ikaharibika kwa mara nyingine. Hatukufika Muzdalifah isipokuwa baada ya jua kuzama. Ni ipi hukumu?

Ibn ´Uthaymiyn: Sijibu swali hili. Haya yalipitika katika mwaka gani?

Muulizaji: Sikumbuki.

Ibn ´Uthaymiyn: Tuchukulie kuwa ni katika mwaka wa mwisho. Ni kwa nini anauliza hivi sasa? Mpaka sasa kumeshapita miezi kumi na moja. Ni kwa nini alichelewesha kuuliza mpaka hivi sasa?

Muulizaji: Ni ipi hukumu?

Ibn ´Uthaymiyn: Hatujibu. Kwa kweli mimi naona kuwa mfano wa watu kama hawa hawastahiki kujibiwa. Isipokuwa ikiwa kama ni mjinga asiyejua chochote. Lakini kwa sura kama hii aliyotaja hakuna yeyote asiyetambua kuwa ina makosa. Alipaswa kuuliza akiwa Makkah kabla hajamaliza hajj yake. Lakini kwa kujengea juu ya kanuni inayotambulika kwa wanachuoni ni kwamba yule ambaye hakuwahi kulala Muzdalifah au angalau kwa uchache akawahi kuja kabla ya alfajiri analazimika kichinjwa ambacho kitachinjwa Makkah na kugawanywa kwa mafukara. Asiyepata hakuna kitu juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (72) http://binothaimeen.net/content/1653
  • Imechapishwa: 06/04/2020