Swali: Je, inafaa kutumia maji ya zamzam kwa ajili ya kupikia au kuogea janaba?

Jibu: Zamzam ni maji yenye kuheshimiwa kwa ajili ya kunywa au kutia wudhuu´ wa kawaida. Si sawa kuyatumia kwa ajili ya janaba au kuyachukulia si lolote si chochote. Ni maji matukufu. Yatumiwe kwa ajili ya kunywa. Kuyatumia kwa ajili ya janaba na mfano wake bora ni kuepuka kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-استعمال-ماء-زمزم-في-الطبخ-أو-الإغتسال-من-الجنابة
  • Imechapishwa: 12/06/2022