Swali: Mama yangu ana nyumba ya Waqf. Kumeshapita muda mrefu juu ya nyumba hii mpaka imekuwa haisilihi kukaa. Ninachotaka ni kuihamisha Waqf na kuuza nyumba hii na niweke thamani yake msikitini, jumuiya ya kheri au njia yoyote miongoni mwa njia za ihsaan. Je, inafaa kwangu kufanya hivo?

Jibu: Haifai kwako kuondoa Waqf hiyo au kuihamisha kwa kitu ambacho hakikuanishwa na mfadhili. Yakiharibika manufaa yake basi itafaa kuhamisha katika kitu mfano wake au kitu kingine kinachosimama nafasi yake kama vile ardhi, dukani au mtende. Hivyo mapato yake yatatolewa juu ya nyumba kusudiwa. Lakini hayo yafanyika kupitia mahakama katika nchi iliopo waqf hiyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (07/20)
  • Imechapishwa: 12/08/2022