Alichukua vitabu vya waqf maktabah, shuleni au msikitini

Swali: Katika miaka yangu ya nyuma ya masomo tulikuwa na maktabah katika shule yetu ambayo inajumuisha vitabu kadhaa na magazeti ambavyo havikuwa vinapewa umuhimu wowote na wanafunzi. Mimi nilikuwa napenda kusoma na kuhifadhi vitabu. Baadhi ya vitabu takriban vinne vya dini, vitabu vya tiba na vitabu vya visa vilivyokuwepo vilinipendeza. Nilivichukua kutoka katika maktabah ya shule ili nivisome na kuvirudilia. Katika kipindi cha masomo yangu nilisahau kuvirudisha maktabah. Baada ya kumaliza shule kwa takriban miaka mitatu dada yangu mmoja alinambia kwamba tukichukua vitabu hivyo na kusivirudishe kwanza ni haramu na pia tutahukumiwa siku ya Qiyaamah. Lakini itambulike kuwa wakati nilipovichukua sikuwa najua hukumu yake na pia waalimu na wanafunzi hawakuwa wakivitilia umuhimu wowote. Mimi nilivichukua ili nifadike navyo na khaswa vile vitabu vya kidini. Sitaki kuvirudisha kwa sababu ndani yake mna hukumu zinazofaidika nazo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni lazima kwako kuvirejesha maktabah kwa sababu vina hukumu moja ya waqf ya maktabah. Haijuzu kwa yeyote kuchukua chochote kutoka katika zile maktabah za ummah wala maktabah za shule isipokuwa baada ya idhini ya wale wanaohusika navyo kwa njia ya kuazima kwa muda maaluum. Ni lazima kwako pamoja na hayo kutubu kwa Allaah kutokana na uliyoyafanya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/353)
  • Imechapishwa: 12/08/2022