Kuhamisha vitabu ambavyo watu hawanufaiki navyo mahali kwengine

Swali: Nimefanya maktabah msikitini kwetu na nikafanya vitabu vilivyomo kuwa ni Waqf. Vimehamwa kwa miaka mingi. Je, inafaa kwangu kuviondosha na kuviweka Waqf mahali kwengine?

Jibu: Ikiwa watu hawanufaiki navyo huko, vihamishe mahali karibu zaidi ambapo watu watanufaika navyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (45)
  • Imechapishwa: 20/07/2024