Mtu anataka kuhamisha nia kutoka katika swalah hii na kwenda kwenye  nyingine. Je, hili linawezekana? Hebu tutazame. Anahama kutoka katika swalah inayopendeza maalum na kwenda katika swalah inayopendeza maalum nyingine au anahama kutoka katika swalah inayopendeza ilyoachiwa na kwenda katika swalah inayopendeza maalum? Si sahihi.

Mfano wa swalah inayopendeza ilyoachiwa, mtu amesimama anataka kuswali swalah inayopendeza ilyoachiwa na katikati ya swalah akakumbuka kuwa hakuswali Raatibah ya Fajr kisha baada ya hapo akainuia kuwa ni Raatibah ya Fajr. Tunasema kuwa haisihi kuiswali kama Raatibah ya Fajr. Kwa sababu ni kuhama kutoka katika swalah inayopendeza ilyoachiwa na kwenda katika swalah inayopendeza maalum. Swalah inayopendeza maalum ni lazima unuie kabla ya kuanza. Ni lazima unuie Raatibah ya Fajr tokea mwanzoni wa Takbiyrat-ul-Ihraam mpaka katika Tasliym.

Mfano wa swalah inayopendeza na kwenda swalah inayopendeza nyingine. Mtu amesimama anataka kuswali ´Aswr na katikati ya swalah amekumbuka kuwa hakuswali Dhuhr au akakumbuka kuwa ameiswali bila ya wudhuu’ kisha sasa akanuia kuiswali Dhuhr. Je, inasihi kuiswali kama Dhuhr au hapana? Haisihi. Kwa kuwa ni kuhama kutoka katikaswalah inayopendeza na kwenda katika swalah inayopendeza maalum nyingine. Vilevile ile swalah yake ya ´Aswr ambayo alikuwa ameshaianza haisihi pia kwa kuwa ameikata kwa kuhamisha nia kwenda Dhuhr. Hivyo, si Dhuhr wala ´Aswr zote hazisihi. ´Aswr haisihi kwa kuwa ameikata. Dhuhr pia haisihi kwa kuwa hakuianza kwa kunuia kama Dhuhr. Swalah ya Dhuhr inaanzishwa tokea katika Takbiyrat-ul-Ihraam mpaka katika salamu.

Ama kuhusu kuhamisha nia kutoka katika swalah inayopendeza maalum na kwenda katika swalah inayopendeza ilyoachiwa, ni sawa. Kwa mfano mtu ameanza kuswali swalah ya faradhi na kisha baada ya kufunga swalah akakumbua kuwa yuko na miadi ambayo hawezi kuichelewesha. Baada ya hapo akainuia kuwa swalah inayopendeza. Ni sahihi endapo wakati ni mpana na mkusanyiko, haitompita.  Kwa sharti hizi mbili:

1 – Ikiwa wakati ni mpana.

2 – Ikiwa mkusanyiko hautompita.

Kwa mfano akiwa ndani ya swalah ya mkusanyiko ni jambo lisilowezekana akahamisha nia kutoka mkusanyiko na kwenda swalah inayopendeza ilyoachiwakwa sababu hili litamfanya yeye kukosa swalah ya mkusanyiko. Hali kadhalika wakati ukiwa mfinyu si sahihi akaihamisha nia kwenda swalah inayopendeza ilyoachiwa kwa kuwa wakati wa swalah ya faradhi haiwezekani ikaswaliwa wakati mwingine ikiwa wakati wake ni mfinyu. Lakini endapo wakati bado ni mpana na swalah ya mkusanyiko imeshampita, ni sawa ukahamisha nia kutoka faradhi na kwenda katika swalah inayopendeza ilyoachiwa na utoe salamu baada ya Rak’ah mbili. Baada ya hapo nenda katika miadi yako na kisha baadaye urudi katika swalah yako ya faradhi. Hivyo kuna aina tatu ya kuhamisha nia kutoka swalah na kwenda nyingine:

1 – Kutoka swalah inayopendeza ilyoachiwa na kwenda katika swalah maalum. Katika hali hii ile swalahmaalum haisihi na swalah ya swalah inayopendeza ilyoachiwa ndio inabaki na ni sahihi.

2 – Kutoka swalah maalum na kwenda swalah maalum. Zote mbili zinabatilika.

3 – Kutoka swalah maalum na kwenda swalah iliyoachiwa. Ni sahihi. Lakini ile maalum itahesabika hajaiswali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/379-381)
  • Imechapishwa: 28/05/2023