Swali: Ni ipi hukumu ya kugeuka ndani ya swalah kwa ajili ya kuomba ulinzi dhidi ya shaytwaan?

Jibu: Kugeuka ndani ya swalah kwa ajili ya kumuomba Allaah kinga dhidi ya shaytwaan aliyefukuzwa mbali wakati wa kuhisi wasiwasi hapana neno. Bali ni kitendo kilichopendekezwa wakati kunapokuwa na haja kubwa ya kufanya hivo. Mtu afanye hivo kwa kichwa peke yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha ´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipomlalamikia yale anayohisi katika wasiwasi wa shaytwaan. Ndipo akamwamrisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ateme cheche za mate upande wa kushoto kwake mara tatu na pia aombe kinga kwa Allaah kutokamana na shaytwaan. Akafanya hivo na Allaah akamponya kutokamana na hayo.

Kuhusu kugeuka ndani ya swalah pasi na haja ni kitu kimechukizwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wakati alipoulizwa juu ya hilo:

“Ni ubadhirifu anaoufanya shaytwaan katika swalah ya mja.”[1]

[1] Imaam Ahmad (13891) na al-Bukhaariy (751).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/130)
  • Imechapishwa: 24/10/2021