Swali: Sisi ni jopo ambalo tumetoka kwenda katika pikniki nchikavu kwa umbali wa 80 km na tumekaa huko siku tatu. Miongoni mwetu wako ambao wamefupisha na kukusanya swalah na wengine hawakufanya hivo. Ni lipi la sawa?
Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba ni sawa kufupisha. Kwa sababu masafa yanaruhusu kufupisha. 80 km ndio mwendo wa siku mbili kwa ngamia aliyebeba vitu. Lakini hata hivyo hakuna haja ya kukusanya. Mnatakiwa mswali kila swalah ndani ya wakati wake. Hivo ndivo wanavofanya mahujaji Minaa ambapo wanafupisha na hawakusanyi. Mtu anakusanya wakati anapohitajia kufanya hivo. Lakini hata hivyo hakuna neno iwapo atakusanya. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya Tabuuk hali yakuwa amekwishatua. Lakini mara nyingi kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba alikuwa hakusanyi isipokuwa anapokuwa njiani. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakusanyi isipokuwa anapokuwa njiani. Ama anapokuwa amekwishatua anaswali kila swalah ndani ya wakati wake hali ya kufupisha bila ya kukusanya.”
Kwa hiyo lililo bora ni kufupisha bila ya kukusanya midhali mtu amekwishatua.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191634
- Imechapishwa: 04/04/2020
Swali: Sisi ni jopo ambalo tumetoka kwenda katika pikniki nchikavu kwa umbali wa 80 km na tumekaa huko siku tatu. Miongoni mwetu wako ambao wamefupisha na kukusanya swalah na wengine hawakufanya hivo. Ni lipi la sawa?
Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba ni sawa kufupisha. Kwa sababu masafa yanaruhusu kufupisha. 80 km ndio mwendo wa siku mbili kwa ngamia aliyebeba vitu. Lakini hata hivyo hakuna haja ya kukusanya. Mnatakiwa mswali kila swalah ndani ya wakati wake. Hivo ndivo wanavofanya mahujaji Minaa ambapo wanafupisha na hawakusanyi. Mtu anakusanya wakati anapohitajia kufanya hivo. Lakini hata hivyo hakuna neno iwapo atakusanya. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikusanya Tabuuk hali yakuwa amekwishatua. Lakini mara nyingi kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba alikuwa hakusanyi isipokuwa anapokuwa njiani. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Hakusanyi isipokuwa anapokuwa njiani. Ama anapokuwa amekwishatua anaswali kila swalah ndani ya wakati wake hali ya kufupisha bila ya kukusanya.”
Kwa hiyo lililo bora ni kufupisha bila ya kukusanya midhali mtu amekwishatua.
Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191634
Imechapishwa: 04/04/2020
https://firqatunnajia.com/kufupisha-swalah-katika-safari-ya-pikniki-umbali-wa-80-km/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)