Swali: Kufungua kifungo cha juu cha kanzu ndani ya swalah ni katika Sunnah?

Jibu: Si Sunnah wala si Bid´ah. Bora kwa mtu asimame mbele ya Allaah akiwa katika hali nzuri. Imepokelewa katika Hadiyth kwamba mtu asujudu kwa mavazi yake na asujudu vilevile kwa nywele zake. Imekuja katika Hadiyth:

“Nimekatazwa kuzifunga nywele au nguo.”

Kilicho Sunnah ni mtu asifunge nywele wala nguo yake[1]. Kwa hivyo usifunge nguo wala kiunganisha cha mkono wa nguo. Ukiwa na nywele usizifunge bali ziache zilale. Vilevile vifungo usivifunge. Kufungua vifungo vya juu kwa sababu ya joto hakuna neno. Kitendo hicho sio Sunnah wala Bid´ah.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/55-sifa-ya-sujuud/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (12) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191546
  • Imechapishwa: 24/08/2019