Inafaa kumuozesha msichana yatima bila ya idhini?

Swali 681: Inafaa kumuozesha msichana yatima bila ya idhini?

Jibu: Msichana mtumzima haozeshwi na kaka yake isipokuwa kwa idhini yake. Idhini ya mwanamke mtumzima ni kwa kuzungumza na kutoa idhini. Idhini ya msichana bikira ni ima kuzungumza au kunyamaza asionyeshe kupinga. Ikiwa mama yake, shangazi yake au dada yake au yeye mwenyewe akasema kuwa ameridhia kabla ya kutamka kwake, basi hakuhitajiki ushahidi juu ya idhini yake. Isipokuwa kukikhofiwa kwamba kaka yake au walii wake anataka kumlazimisha kuolewa, basi hapo itakuwa ni lazima kutoa ushahidi juu ya idhini yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 265
  • Imechapishwa: 24/08/2019