Kufunga swawm ya ´Arafah iliyoangukia siku ya ijumaa

Swali: Nilifunga siku ya ´Arafah iliyoangukia siku ya ijumaa na sikufunga siku moja kabla yake alkhamisi. Je, nimepata dhambi?

Jibu: Tunataraji kuwa huna dhambi. Hukukusudia kuifunga peke yake, bali uliifunga kwa sababu ni siku ya ´Arafah. Hata hivyo ungefunga pamoja nayo siku moja kabla yake alkhamisi ingelikuwa tahadhari zaidi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kufunga siku ya ijumaa peke yake kwa ambaye anafunga swawm iliyopendekezwa. Wewe unafunga swawm iliyopendekezwa. Kama tulivosema tahadhari zaidi ni kufunga  siku ya moja kabla yake alkhamisi hata kama makusudio yako ni kufunga siku ya ´Arafah. Lakini kile kitendo cha muumini kujitahidi kuafikiana na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutekeleza yale aliyoamrisha ndio salama na tahadhari zaidi. Hata hivyo haijuzu kufunga ijumaa peke yake kwa kukusudia ubora wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo. Lakini tunatumai kuwa hapati dhambi akifunga ijumaa kwa sababu ´Arafah imeangukia siku hiyo. Lakini salama na tahadhari zaidi ni yeye kufunga siku ya moja kabla yake ambayo ni alkhamisi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.binbaz.org.sa/mat/13717
  • Imechapishwa: 06/07/2022