Kufunga safari kwenda Makkah na Madiynah kuswali Tarawiyh

Swali: Ni ipi hukumu ya kupanga safari kwenda Makkah na Madiynah kwa lengo la kuhudhuria ukhitimishaji wa Qur-aan?

Jibu: Kupanga safari kwenda Makkah na Madiynah ni kujikurubisha na kumtii Allaah. Ni mamoja kwa ajili ya ´Umrah au kuswali ndani ya msikiti Mtakatifu au kuswali katika msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Ramadhaan na wakati mwingine. Hilo ni kwa maafikiano ya waislamu. Hapana neno kufanya hivo. Kwa sababu kuhudhuria ukhitimishaji ni miongoni mwa mambo yanayofanywa katika misikiti Mitukufu miwili na pengine akajaaliwa pia kufanya ´Umrah, inakuwa kheri juu ya kheri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/361)
  • Imechapishwa: 07/11/2021