Kufuatilia ile misikiti inayokhitimisha Qur-aan

Swali: Ni upi hukumu ya kupeleleza ni misikiti ipi inayokhitimisha Qur-aan?

Jibu: Hili lina sababu zake. Akiwa na matumaini ya kukubaliwa du´aa. Kwa sababu Allaah (Jalla wa ´Alaa) ameahidi kuitikia. Anaweza kumkubalia huyu na asimkubalie mwengine. Ambaye anahamahama kwenda katika misikiti ikiwa malengo yake ni kheri, basi huenda akaingia ndani ya hawa wenye kuitikiwa. Anataraji kwamba Allaah anawaitikia na kuwa pamoja nao. Kwa hivyo hapana neno kufanya hivo akiwa na nia njema na lengo zuri. Kuna matarajio Allaah akamnufaisha kwa hilo na zikakubaliwa du´aa zao ilihali yeye yuko pamoja nao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/360)
  • Imechapishwa: 07/11/2021