Kufuga ndege na kuwaweka ndani ya banda

Swali: Ni ipi hukumu ya kufuga ndege na kuwaweka kwenye mabanda hawatoki humo huku wakipewa chakula na kinywaji?

Jibu: Hakuna ubaya katika hilo. Ndege katika vizimba pamoja na kuwafanyia wema na kutowapuuza, hakuna tatizo. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akipita kwa mtoto wa Abu Twalhah – ndugu yake Anas kwa mama yake – alikuwa na ndege anayeishika na kucheza nayo, na alikuwa akisema:

”Nini kimemtokea an-Nughayr, ee Abu ´Umayr?”

Kwa hiyo kushika ndege na kuwaweka majumbani ni jambo la zamani. Hakuna ubaya ikiwa ndege wanatunzwa na haki zao hazipuuzwi.

Swali: Kuna wengine ni ndege wakali wanauzwa wanaitwa ndege wa mapambo?

Jibu: Siwajui, kwa vyovyote vile hakuna ubaya ikiwa wamewindwa na hawamdhuru yeyote.

Swali: Ikiwa wanazuiliwa uhuru wao na hatimaye wanakufa ndani ya kizimba, kwa sababu wanahisi kunyimwa uhuru wao na kuruka angani?

Jibu: Hapana, hawafi. Tunajua ndege hadi sasa kwa miaka mingi wako hai.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3380/حكم-اقتناء-الطيور-وحبسها-في-اقفاص
  • Imechapishwa: 16/09/2026