Swali: Mimi na familia yangu tunaishi katika jengo la ghorofa na katika jengo hili anaishi kwenye ghorofa ya pili mtu wa Druze kutoka Lebanon. Nikamwamrisha mwanawe aswali msikitini na hilo nikalifanya mara nyingi, lakini sikupata majibu kutoka kwao. Nikazungumza na baba yake ambaye alisema kuwa wao ni Druze, tunaamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Wake, na kwamba tunashuhudia kwamba Muhammad ni mwisho wa Manabii, kisha akanitajia faradhi zote za Uislamu na anasema kwamba wakati mwingine anaswali na wenzanke kazini, ambao ni wasaudi, lakini akasema kuwa wao wako sehemu yao ya faragha na mazungumzo yakawa marefu naye. Sasa sijui nifanye nini, je, tunaruhusiwa kumtoa katika jengo? Ikiwa atakataa kutoka, je, tunaruhusiwa kubaki naye katika jengo hali ya kuwa najua kwamba wao si waislamu? Naomba mwongozo wenu.

Jibu: Druze ni miongoni mwa watu wanaoficha sana yale waliyo nayo, kujisitiri juu ya dini yao na kutoifichua kwa watu. Wao si pamoja na waislamu. Wao hujionyesha kwamba wao si waislamu. Kinachojulikana kuwahusu ni kwamba wao ni washirikina na kwamba wao ni waabudu wa al-Haakim al-´Ubaydiy. Hawako pamoja na waislamu na wala dhahiri yao si pamoja na waislamu. Kinachojulikana kwa wanaowajua ni kwamba wao si waislamu wala hawafuati dini ya Uislamu. Wana ´ibaadah zilizo nje ya yale waliyo nayo waislamu na wana uhusiano na al-Haakim al-´Ubaydiy anayejulikana. Hivi ndivyo walivyotajwa na wanaowajua.

Lakini kuwapa nasaha ni muhimu, kuwapa nasaha, kuwalingania kwa Allaah, kuwaelekeza katika kheri na kuwafundisha yale yatakayowanufaisha. Huenda Allaah akawaongoza. Ni kama wanavyolinganiwa washirikina wengine na mayahudi na manaswara. Yeyote aliye na dhahiri ya shari analinganiwa. Vivyo hivyo anayejulikana kwa shari. Vivyo hivyo anayejulikana kwa ´Aqiydah potofu iliyopotoka na asiyeenda pamoja na waislamu katika matendo yao na haswali pamoja nao ananasihiwa na kuelekezwa katika kheri na kufundishwa. Huenda Allaah akamuongoza kwa sababu zako. Ama kuhusu wewe kuhama jengo kwa ajili yake, hapana, muda wa kuwa yeye yuko ghorofa na wewe uko ghorofa nyingine hakuna madhara. Nasaha ndiyo inayotakiwa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3363/بيان-ما-عليه-الدورز-من-العقيدة-وواجبنا-نحوهم
  • Imechapishwa: 16/09/2026