142 – ´Abdullaah bin al-Haytham ametukhabarisha: Hishaam bin ´Abdil-Malik ametukhabarisha: Hammaad bin Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Kinaanah bin Nu´aym, kutoka kwa Abu Barzah, aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alikutana na maadui na akasema: “Je, kuna mtu mmemkosa?” Wakasema: ”Ndio, tunamkosa fulani na fulani na fulani. Akasema mara ya pili: “Je, kuna mtu mmemkosa?” Wakasema: ”Hapana.” Ndipo akasema: ”Namkosa Julaybiyb. Ondokeni mkamtafute miongoni mwa waliouliwa.” Tahamaki ikaonekana kwamba alikuwa amelala maiti pembezoni na wale saba ambao yeye aliwaua, ambapo na wao wakamuua. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akapewa taarifa ambapo akaja mwenyewe maeneo yale, akasimama juu yake na akasema: “Huyu anatokana nami, nami natokana naye. Amewaua saba kisha nao wakamuua. : “Huyu anatokana nami, nami natokana naye. Amewaua saba kisha nao wakamuua.” Alisema hivo mara mbili. Kisha akambeba mikononi mwake. Hakuwa na machela mengine isipokuwa mikono ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Baada ya hapo akazikwa bila kuoshwa.”[1]

[1] Muslim (2472).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 100
  • Imechapishwa: 16/09/2026