Kufanya Tayammum kwa ambaye yuko pikniki kutokana na uchache wa maji

Swali: Baadhi ya waislamu katika masiku ya likizo wanatoka nje ya mji wa ar-Riyaadh kwa ajili ya pikniki bila kunuia safari na wanabeba maji kidogo. Unapofika wakati wa swalah wanafanya Tayammum badala ya kutumia maji kwa hoja ya uchache wa maji. Pamoja na kuzingatia kwamba wanaweza kutafuta maji au wakayabeba kipindi cha safari. Je, inafaa kwao kufanya Tayammum katika hali hii? Ikiwa haifai ni ipi hukumu ya kuswali pasi na kutawadha?t

Jibu: Wakitoka kwa ajili ya pikniki na ukafika wakati wa swalah na wasiwe isipokuwa na maji kidogo kwa kiwango cha haja yao na maji yako mbali nao, wataswali kwa Tayammum. Lakini wakibeba pamoja nao itakuwa ndio bora ikiwa kuna wepesi wa kufanya hivo. Maji yakiwa karibu nao basi itawalazimu kutawadha. Ikiwa yako mbali nao na kuna ugumu kwao kuyaendea au watapoteza wakati wao kwa kuwa kwake mbali, basi hapana vibaya wakayafanya Tayammum. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah walikuwa wakifanya Tayammum pindi maji yanapokuwa mbali nao.

Kuhusu swalah ya ijumaa haiwalazimu ikiwa wako mbali na mji na hawasikii adhaana. Umbali weneywe ni ule usiopungua chini ya takriban mita 5541.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/202)
  • Imechapishwa: 26/09/2021