Swali: Nina watoto washirika wanaofanya kazi ya kuuza diski. Huwa wanaweka katika boksi diski thelathini na tano. Mteja anapokuja humwambia kuwa zimo khamsini. Hali hii ndivyo ilivyo kwa wauzaji wote wa diski. Ni yepi maoni yenu kuhusu hilo?
Jibu: Hili ni ghushi, khiyana na uongo. Yule anayehifadhi katika boksi diski thelathini na tano kisha akamwambia mnunuzi kuwa zimo khamsini au arobaini, amefanya jambo lililoharamishwa na ni uovu. Ni wajibu kwake atubie kwa Allaah na atoe swadaqah kiasi kinacholingana na alichokichukua katika mali za watu bila haki, kwa sababu kufanya hivo ni ghushi. Wajibu ni kusema ukweli kuhusu kilichomo katika boksi; ikiwa ni kumi aseme ni kumi, ikiwa ni arobaini aseme ni arobaini, asiongeze. Hivyo ndivyo wajibu ulivyo. Ikiwa ameongeza, basi amedanganya, amekosea na amewadanganya waislamu. Kwa hiyo ni wajibu kwake atubie kwa Allaah na arudishe ziada kwa mwenye mali ikiwa anamjua. Ikiwa hamjui, basi atoe swadaqah ile ziada aliyochukua bila haki.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1882/حكم-الغش-في-البيع
- Imechapishwa: 04/07/2026
Swali: Nina watoto washirika wanaofanya kazi ya kuuza diski. Huwa wanaweka katika boksi diski thelathini na tano. Mteja anapokuja humwambia kuwa zimo khamsini. Hali hii ndivyo ilivyo kwa wauzaji wote wa diski. Ni yepi maoni yenu kuhusu hilo?
Jibu: Hili ni ghushi, khiyana na uongo. Yule anayehifadhi katika boksi diski thelathini na tano kisha akamwambia mnunuzi kuwa zimo khamsini au arobaini, amefanya jambo lililoharamishwa na ni uovu. Ni wajibu kwake atubie kwa Allaah na atoe swadaqah kiasi kinacholingana na alichokichukua katika mali za watu bila haki, kwa sababu kufanya hivo ni ghushi. Wajibu ni kusema ukweli kuhusu kilichomo katika boksi; ikiwa ni kumi aseme ni kumi, ikiwa ni arobaini aseme ni arobaini, asiongeze. Hivyo ndivyo wajibu ulivyo. Ikiwa ameongeza, basi amedanganya, amekosea na amewadanganya waislamu. Kwa hiyo ni wajibu kwake atubie kwa Allaah na arudishe ziada kwa mwenye mali ikiwa anamjua. Ikiwa hamjui, basi atoe swadaqah ile ziada aliyochukua bila haki.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1882/حكم-الغش-في-البيع
Imechapishwa: 04/07/2026
https://firqatunnajia.com/kufanya-ghushi-katika-biashara/