Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth inayosema:
“Hakuna swalah wakati chakula kimetengwa wala wakati anazuia haja ndogo au kubwa.”?
Jibu: Hadiyth ni Swahiyh:
“Hakuna swalah wakati chakula kimetengwa wala wakati anazuia haja ndogo au kubwa.”
Swali: Je, swalah ya anayeswali katika hali hiyo ni sahihi?
Jibu: Swalah yake ni sahihi, lakini amekosea. Ikiwa anapambana na haja, inampasa aanze na haja ndogo au kubwa, hata kama atakosa swalah ya mkusanyiko. Aende akatimize haja yake, kisha aswali peke yake kwa unyenyekevu. Swalah kwa unyenyekevu ukiwa peke yako ni bora kuliko swalah bila unyenyekevu hata kama uko na imamu.
Swali: Lakini swalah yake bado ni sahihi?
Jibu: Ndio, swalah yake ni sahihi. Lakini amefanya jambo lisilopasa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1889/ما-صحة-حديث-لا-صلاة-بحضرة-طعام
- Imechapishwa: 04/07/2026
Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth inayosema:
“Hakuna swalah wakati chakula kimetengwa wala wakati anazuia haja ndogo au kubwa.”?
Jibu: Hadiyth ni Swahiyh:
“Hakuna swalah wakati chakula kimetengwa wala wakati anazuia haja ndogo au kubwa.”
Swali: Je, swalah ya anayeswali katika hali hiyo ni sahihi?
Jibu: Swalah yake ni sahihi, lakini amekosea. Ikiwa anapambana na haja, inampasa aanze na haja ndogo au kubwa, hata kama atakosa swalah ya mkusanyiko. Aende akatimize haja yake, kisha aswali peke yake kwa unyenyekevu. Swalah kwa unyenyekevu ukiwa peke yako ni bora kuliko swalah bila unyenyekevu hata kama uko na imamu.
Swali: Lakini swalah yake bado ni sahihi?
Jibu: Ndio, swalah yake ni sahihi. Lakini amefanya jambo lisilopasa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1889/ما-صحة-حديث-لا-صلاة-بحضرة-طعام
Imechapishwa: 04/07/2026
https://firqatunnajia.com/swalah-ya-anayeswali-hali-ya-kubanwa-na-haja/