Swali: Je, Anaashiyd ni njia miongoni mwa njia za kufanya Da´wah?

Jibu: Hakuna mambo ya Anaashiyd za Kiislamu. Kuzipachika jina kwamba ni za “Kiislamu” hili ni kosa. Afadhali waseme “Anaashiyd” tu. Hili ni kwa Suufiyyah. Anaashiyd ni Dini yao. Ama Ahl-us-Sunnah, hawana Anaashiyd za Kiislamu, kamwe!

Lakini wako na mashairi. Mashairi yalikuwa yakisomwa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna tofauti kati ya shairi na Anaashiyd. Mashairi yanajuzu. Ama Anaashiyd ni jambo limezushwa katika Dini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=yzZUjphdczs
  • Imechapishwa: 10/11/2014