Swali: Unasemaje juu ya mwenye kupiga picha vibonzo vya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambavyo vimefanywa na gazeti la Denmark na anazieneza kwa watu kwa hoja ya kwamba watu waone kitendo hichi kiovu ili aweze kukikataza?

Jibu: Wakati mwingine kukataza maovu kwa dhati yake inakuwa ni maovu. Kueneza picha hizi haijuzu. Haijuzu kueneza picha hizi. Lililo la wajibu ni kuziharibu na kumchukulia hatua. Mtu asizieneze kwa hali yoyote ile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (02) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2105
  • Imechapishwa: 30/06/2020