Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuendelea kunyoa ndevu na anasema kuwa ni Sunnah?

Jibu: Ni haramu. Kunyoa ndevu ni haramu. Mwenye kuendelea kuzinyoa anaendelea kufanya kitendo cha haramu. Kitendo hichi kitamtoa katika haramu na kumpeleka katika dhambi kubwa ikiwa ataendelea kufanya hivo. Ni juu yake kumcha Allaah (´Azza wa Jall) na aziache ndevu zake kwa kumtii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Ziacheni ndevu.”

”Zirefusheni ndevu.”

”Zifugeni ndevu.”

Haya ni maamrisho kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vipi basi atamuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Ziache ndevu zako ndio mapambo yako. Himdi zote za Allaah ndevu ni mapambo na ni ukamilifu kwa mwanaume. Isitoshe ndevu ni kitu kinachomtofautisha yeye na mwanamke.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14763
  • Imechapishwa: 21/06/2020