Kuchukua zakaah ili kuongeza mke mwingine

Swali: Je, inajuzu kwangu kuchukua katika zakaah ya mali ili niweze kuoa mke wa pili kwa kuwa mke wangu hataki kuzaa kutokana na maradhi na mimi najikhofia juu ya nafsi yangu fitina na ninaamini kuzaa mtoto mwema?

Jibu: Ikiwa haya ndio makusudio na mke wako amefikwa na kitu kinachomfanya hawezi kushika mimba na wewe unataka mtoto na huna uwezo wa kuoa mke wa pili, unaweza kuchukua zakaah.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-4-3.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020