Eda kwa mwanamke aliyekufa wakati wa magomvi na mume wake  

Swali: Kulitokea tatizo kati ya mtu na mke wake mpaka mambo yakafikia kumpiga mke wake kisha akawa ameenda kwa familia yake. Mke yule akamuomba mume kujivua katika ndoa na mume akawa amekataa hilo. Wakati walipokuwa katika kuvutana huko mwanaume yule akawa amekufa. Je, mwanamke yule ni lazima akae eda au hapana?

Jibu: Ndio. Maadamu hakumtaliki bado ni mke wake. Ni lazima kwake kukaa eda na atarithi kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-4-3.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020