Swali: Je, kufanya Da´wah na kwenda katika miji ya makafiri na ya waislamu na kueneza Sunnah ni katika Jihaad katika njia ya Allaah?

Jibu: Ndio, ni aina ya Jihaad. Hili linaitangulia Jihaad. Kulingania katika dini ya Allaah kunatangulia kabla ya Jihaad. Kinachotangulia ni kulingania katika dini ya Allaah kisha ndio kunakuja Jihaad. Bila ya shaka hii ni katika aina bora ya Jihaad.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-2-27.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020