Kuchukua maji mapya kwa ajili ya kuosha masikio

Swali: Ni lazima kwa mwenye kutawadha kuchota maji mengine kwa ajili ya masikio yake?

Jibu: Sio lazima kuchukua maji mapya kwa ajili ya masikio. Bali haikupendekezwa kwa mujibu wa maoni sahihi. Kwa sababu namna zote zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hazikutaja ya kwamba alikuwa akichukua maji mapya kwa ajili ya kuosha masikio yake. Bora ni mtu kuyafuta masikio yake kwa mabaki ya maji yaliyobaki baada ya kukifuta kichwa chake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/141)
  • Imechapishwa: 30/06/2017