Kuchukua kutoka katika pesa ya zakaah na kulipa deni unalodaiwa

Swali 339: Mtu ambaye ana deni la kulipa kwa awamu na anaweza kulilipa kupitia mshahara wake. Je, anaweza kuchukua kutoka katika zakaah na kumpa mwenye deni lake mara moja?

Jibu: Ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Muda wa kuwa anaweza kulipa basi yeye ni tajiri[1].

[1] Shaykh wetu Ibn ´Uthaymiyn aliulizwa swali kama hilo ambapo akasema kuwa inafaa akachukua kutoka katika zakaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 119
  • Imechapishwa: 31/05/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´