Swali: Imekuwa ni jambo la kawaida miongoni mwa wanawake kujitunza kwa kuchubua uso kwa kutumia krimu na mafuta. Wakati mwingine ngozi ya uso inaweza kuhusisha upasuaji wa plastiki chini ya anesthesia. Madhumuni ya kuchubua uso ni kuondoa chunusi na makovu kwa ajili ya kupendeza zaidi. Mara nyingine upasuaji wa plastiki unaweza kuwa na matokeo mabaya kama vile kudhihiri alama ya kuungua au chunusi zilizobaki na mengineyo. Ni yepi maoni yako juu ya jambo hili? Je, inazingatiwa ni katika kubadilisha maumbile ya viumbe ya Allaah au ni aina fulani tu ya mapambo? Ni upi usahihi wa Hadiyth:

“Allaah amemlaani mwanamke anayechubua na anaombwa kuchubuliwa.”?

Je, imethibiti kuwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amekataza kujichubua uso kwa kutumia zafarani au kitu kingine?

Jibu: Ikiwa jambo hilo linafanywa kwa lengo la kujipamba, basi ni haramu kama ilivyo kuchonga nyusi, kujichanja na mfano wake. Na ikiwa lengo ni kuondoa kasoro kama vile tundu, rangi nyeusi kwenye ngozi na mfano wake, basi hapana vibaya. ´Arajah bin As´ad (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Pua yangu ilikatwa siku ya Kulaab kabla kipindi kabla ya kuja Uislamu. Hivyo nikachukua pua bandia ya dhahabu. Baada ya kuoza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaniamrisha kuweka pua ya dhahabu.”[1]

Kuhusu Hadiyth, sijui chochote juu yake. Wala sidhani kama imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wala sijui chochote juu ya hayo masimulizi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Ahmad (5/23), Abu Daawuud (4232) na at-Tirmidhiy (1770) aliyesema:

”Hadiyth ni nzuri na geni.”

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/19-20)
  • Imechapishwa: 16/06/2026