Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
142- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:
أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم دخل عَلَيْهَا وعِندها امرأةٌ، قَالَ: (مَنْ هذِهِ؟) قَالَتْ: هذِهِ فُلاَنَةٌ تَذْكُرُ مِنْ صَلاتِهَا. قَالَ: (مهْ، عَلَيْكُمْ بِمَا تُطِيقُونَ، فَواللهِ لا يَمَلُّ اللهُ حَتَّى تَمَلُّوا، وكَانَ أَحَبُّ الدِّينِ إِلَيْهِ مَا دَاوَمَ صَاحِبُهُ عَلَيهِ) مُتَّفَقٌ عَلَيه
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwake na yuko pamoja na mwanamke [mwenzake]. Akamuuliza: “Nani huyu?” Akamwambia: “Huyu ni fulani. Akataja kuhusu swalah zake [anavoswali sana].” Akamwambia: “Koma!” Fanyeni mnachoweza. Ninaapa kwa Allaah kuwa Allaah hachoki mpaka nyinyi mchoke. Kinachopendeza zaidi Kwake ni kile ambacho mwenye nacho anadumu juu yake.”[1]
Kuchoka kwa Allaah sio kama kuchoka kwetu sisi. Kuchoka kwetu ni kwa kutaabika na kuzembea. Lakini kuchoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) ni sifa maalum inayolingana na Yeye. Allaah hafikwi na kutaabika wala kuzembea. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ
“Hakika Tumeumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yake katika siku sita na wala hatukuguswa na uchovu wowote.” (50:38)
Mbingu hizi kubwa na ardhi na vilivyomo ndani yake Allaah ameviumba mnamo siku sita; jumapili, jumatatu, jumanne, jumatano, alkhamisi na ijumaa. Kisha akasema:
وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ
“… na wala hatukuguswa na uchovu wowote.”
bi maana hatukuchoka kwa muda huu mfupi pamoja na ukubwa wake.
[1] al-Bukhaariy na Muslim
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/213-214)
- Imechapishwa: 15/09/2024
Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
142- ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:
أنَّ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم دخل عَلَيْهَا وعِندها امرأةٌ، قَالَ: (مَنْ هذِهِ؟) قَالَتْ: هذِهِ فُلاَنَةٌ تَذْكُرُ مِنْ صَلاتِهَا. قَالَ: (مهْ، عَلَيْكُمْ بِمَا تُطِيقُونَ، فَواللهِ لا يَمَلُّ اللهُ حَتَّى تَمَلُّوا، وكَانَ أَحَبُّ الدِّينِ إِلَيْهِ مَا دَاوَمَ صَاحِبُهُ عَلَيهِ) مُتَّفَقٌ عَلَيه
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwake na yuko pamoja na mwanamke [mwenzake]. Akamuuliza: “Nani huyu?” Akamwambia: “Huyu ni fulani. Akataja kuhusu swalah zake [anavoswali sana].” Akamwambia: “Koma!” Fanyeni mnachoweza. Ninaapa kwa Allaah kuwa Allaah hachoki mpaka nyinyi mchoke. Kinachopendeza zaidi Kwake ni kile ambacho mwenye nacho anadumu juu yake.”[1]
Kuchoka kwa Allaah sio kama kuchoka kwetu sisi. Kuchoka kwetu ni kwa kutaabika na kuzembea. Lakini kuchoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) ni sifa maalum inayolingana na Yeye. Allaah hafikwi na kutaabika wala kuzembea. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ
“Hakika Tumeumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yake katika siku sita na wala hatukuguswa na uchovu wowote.” (50:38)
Mbingu hizi kubwa na ardhi na vilivyomo ndani yake Allaah ameviumba mnamo siku sita; jumapili, jumatatu, jumanne, jumatano, alkhamisi na ijumaa. Kisha akasema:
وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ
“… na wala hatukuguswa na uchovu wowote.”
bi maana hatukuchoka kwa muda huu mfupi pamoja na ukubwa wake.
[1] al-Bukhaariy na Muslim
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/213-214)
Imechapishwa: 15/09/2024
https://firqatunnajia.com/kuchoka-kwa-allaah-sio-kama-viumbe/