Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

144 – Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimuliakuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

هَلَكَ المُتَنَطِّعُونَ

“Wameangamia wapetukaji mipaka. Alisema hivo mara tatu.””[1]

Miongoni kwa kuvuka mipaka ni mtu kujifanyia uzito juu ya nafsi yake katika swalah, swawm na mengine ambayo Allaah amemuwekea wepesi. Akijifanyia uzito mwenyewe katika yale ambayo Allaah amemsahilishia, basi ni mwenye kuangamia. Moja katika hayo ni yale yanayofanywa na baadhi ya wagonjwa na khaswa hufanya hivi katika Ramadhaan, basi Allaah amewaruhusu kula katika hali ya ugonjwa na mtu anakuwa ni mwenye kuhitaji kula na kunywa, lakini hata hivyo mtu anajiwekea ugumu mwenyewe na anafunga. Watu kama hawa tunawaambia kuwa Hadiyth hii inawagusa:

“Wameangamia wapetukaji mipaka.”[2]

[1]Muslim (2670).

[2]Muslim (2670).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/219)
  • Imechapishwa: 15/09/2024