Swali: Ni ipi hukumu ya kuchinja Udhhiyah kwa kisu cha umeme?

Jibu: Sijui kisu cha umeme. Hapana vibaya ikiwa kisu hicho cha umeme, baada ya kutaja jina la Allaah, kinakata koo na mishipa ya pumzi na kinakata vyema. Na ikiwa ni kisu cha kihakika ambacho kinakata koo na mishipa ya pumzi, ni mamoja mtu akachinja kwa kisu cha umeme, kisu cha kawaida,  baada ya kutaja jina la Allaah, amtaje Allaah kisha afanye kazi. Hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/8714/حكم-ذبح-الاضحية-وغيرها-بالسكين-الكهرباىية
  • Imechapishwa: 07/06/2024