Swali: Hadiyth ya ´Aaishah kuhusu kuoga josho la janaba inasema mwishoni mwake:
“…. kisha aoshe miguu yake baada ya kutawadha.”
Je, acheleweshe kuosha miguu yake?
Jibu: Ndio bora. Atawadhe wudhuu´ kamili kwanza, kisha aoge, kisha aoshe miguu yake kwa njia ya ukamilifu baada ya kuisafisha na uchafu wa mwili na mengineyo. Imepokelewa pia akitawadha na akaacha kuosha miguu yake mpaka atapomaliza kuoga kisha baada ya hapo ndio akaiosha. Hayo yamesimuliwa katika Hadiyth ya Maymuunah na katika Hadiyth ya ´Aaishah. Hata hivyo lililo kamili zaidi ni yeye atawadhe wudhuu´ kamili kisha aioshe muosho mwingine. Hilo ndio bora zaidi.
Swali: Baadhi ya wanazuoni wanasema kuwa hilo linapingana na Hadiyth Swahiyh (شاذ) kwa sababu kutakuwa hakuna maana ya kuosha miguu miwili?
Jibu: Hapana, halipingana na Hadiyth Swahiyh. Ni jambo limethibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23017/حكم-تاخير-غسل-الرجلين-في-غسل-الجنابة
- Imechapishwa: 15/10/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)