Kuchelewesha Dhuhr kwa sababu ya joto kali

Swali: Je, imewekwa katika Shari´ah kuchelewesha swalah ya Dhuhr wakati wa majira ya joto pamoja na kuwa misikiti ina kiyoyozi?

Jibu: Ndio. Njiani wakati wa kwenda huko kuna joto. Na si kwamba misikiti yote ina kiyoyozi. Dhuhr icheleweshwe ili kuwe na baridi kidogo. Hii ni Sunnah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika joto kali unatokamana na mvuke wa Jahannam. Kukiwa na joto kali basi  pateni baridi kwa swalah.”[1]

[1] al-Bukhaariy (535).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (89) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20%D9%85%D9%86%20%D9%85%D8%B5%D8%A7%D9%8A%D8%AF%20%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%8A%D8%B7%D8%A7%D9%86-08-07-1439.lite__0.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2018