Swali: Ni ipi hukumu ya kucheka ndani ya swalah? Je, mtu akicheka katika swalah anatakiwa kuirudia?
Jibu: Kucheka katika swalah kunabatilisha swalah kwa maafikiano ya wanazuoni. Hivyo ikiwa mtu atacheka katika swalah, basi swalah yake inabatilika. Vivyo hivyo ikiwa atasema maneno kwa makusudi, swalah yake inabatilika. Lakini ikiwa atasema kwa kusahau au kwa ujinga, basi swalah ya aliyesahau au asiyejua haibatiliki. Ama kucheka, kunabatilisha swalah kwa hali zote. Kwa sababu ni kudharau swalah na kuonesha kuifanyia wepesi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/348)
- Imechapishwa: 14/03/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kucheka ndani ya swalah? Je, mtu akicheka katika swalah anatakiwa kuirudia?
Jibu: Kucheka katika swalah kunabatilisha swalah kwa maafikiano ya wanazuoni. Hivyo ikiwa mtu atacheka katika swalah, basi swalah yake inabatilika. Vivyo hivyo ikiwa atasema maneno kwa makusudi, swalah yake inabatilika. Lakini ikiwa atasema kwa kusahau au kwa ujinga, basi swalah ya aliyesahau au asiyejua haibatiliki. Ama kucheka, kunabatilisha swalah kwa hali zote. Kwa sababu ni kudharau swalah na kuonesha kuifanyia wepesi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/348)
Imechapishwa: 14/03/2026
https://firqatunnajia.com/kucheka-ndani-ya-swalah/