Kuchanganyika na mwenye magonjwa ya kuambukiza

Swali: Je, mtu anapata dhambi akikaa na mwenye ukoma au akakaa na mtu mwenye ugonjwa wa upele hali ya kumtegemea Allaah?

Jibu: Hapana vibaya ikiwa amefanya hivo kutokana na manufaa. Ni kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipomjilia mwenye ukoma:

بسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

Amefanya hivo kwa kumtegemea Allaah na akala pamoja naye. Kufanya sababu ni jambo linatakikana. Mtu akihitaji kuchanganyika na mgonjwa ili amhudumie au amtibu hapana vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22027/حكم-مخالطة-المجذوم-والمريض-لحاجة
  • Imechapishwa: 15/10/2022