Kuchanganya Takbiyrat-ul-Ihraam na ya kwenda Rukuu´

Swali: Ni ipi hukumu ya kujumuisha kati ya Takbiyrat-ul-Ihraam na Rukuu´ katika swalah?

Jibu: Piga Takbiyrat-ul-Ihraam hali ya kuwa umesimama na usinuie ikawa ndio ya Rukuu´. Leta Takbiyrat-ul-Ihraam hali ya kuwa umesimama kwa sababu ni nguzo miongoni mwa nguzo za swalah.

Kuhusiana na Takbiyr ya kwenda kwenye Rukuu´ katika hali hii sio wajibu. Ukitaka utaileta na usipotaka hutoileta.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14763
  • Imechapishwa: 21/06/2020