Swali: Imekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya watu, na khaswa wanawake, kuanza kupaka ngozi zao kemikali na vitu vya asili ambavo vinaibadilisha rangi ya ngozi. Baadhi ya waume wanawaamrisha wake zao kupaka ngozi zao na kusema kwamba wake ni wajibu kwa mwanamke kumpambia mume wake. Je, kuna makatazo yoyote kwa upande wa Shari´ah?
jibu: Ikiwa kunaibadilisha ngozi kwan njia ya kudumu ni haramu na bali ni miongoni mwa madhambi makubwa. Kwa sababu ni mabadiliko makubwa ya maumbile ya Allaah (Ta´ala) kuliko kuchanja. ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amemlaani mwanamke mwenye kufanya chanjo na mwanamke mwenye kufanywa chanjo, mwanamke mwenye kuchonga nyusi na mwanamke mwenye kuchongwa nyusi na mwanamke mwenye kufanya mwanya kwa ajili ya kutafuta urembo wanaoyabadilisha maumbile ya Allaah.”
Kisha akasema:
“Je, nisimlaani yule aliyelaaniwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall)?”[1]
Lakini ikiwa mabadiliko sio kwa njia ya kudumu, kama vile hina, wanja na rangi ya mdomo, hapana vibaya. Kwa hivyo ni wajibu kujihadhari na kutahadharisha kutokamana na kubadilisha maumbile ya Allaah. Ni lazima kwa ummah utahadharishwe ili kusienee maovu na ikakita na hivyo ikawa ni vigumu kujirejea kitendo hicho.
[1] al-Bukhaariy (5934) na Muslim (2125).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/20-21)
- Imechapishwa: 15/07/2026
Swali: Imekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya watu, na khaswa wanawake, kuanza kupaka ngozi zao kemikali na vitu vya asili ambavo vinaibadilisha rangi ya ngozi. Baadhi ya waume wanawaamrisha wake zao kupaka ngozi zao na kusema kwamba wake ni wajibu kwa mwanamke kumpambia mume wake. Je, kuna makatazo yoyote kwa upande wa Shari´ah?
jibu: Ikiwa kunaibadilisha ngozi kwan njia ya kudumu ni haramu na bali ni miongoni mwa madhambi makubwa. Kwa sababu ni mabadiliko makubwa ya maumbile ya Allaah (Ta´ala) kuliko kuchanja. ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amemlaani mwanamke mwenye kufanya chanjo na mwanamke mwenye kufanywa chanjo, mwanamke mwenye kuchonga nyusi na mwanamke mwenye kuchongwa nyusi na mwanamke mwenye kufanya mwanya kwa ajili ya kutafuta urembo wanaoyabadilisha maumbile ya Allaah.”
Kisha akasema:
“Je, nisimlaani yule aliyelaaniwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall)?”[1]
Lakini ikiwa mabadiliko sio kwa njia ya kudumu, kama vile hina, wanja na rangi ya mdomo, hapana vibaya. Kwa hivyo ni wajibu kujihadhari na kutahadharisha kutokamana na kubadilisha maumbile ya Allaah. Ni lazima kwa ummah utahadharishwe ili kusienee maovu na ikakita na hivyo ikawa ni vigumu kujirejea kitendo hicho.
[1] al-Bukhaariy (5934) na Muslim (2125).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/20-21)
Imechapishwa: 15/07/2026
https://firqatunnajia.com/kubadilisha-rangi-ya-ngozi/