Jambo la nne unaoonesha ubatili wa ´Aqiydah ya wanaokanusha sifa ni kubainisha kwamba akili timamu iliyosalimika kutokana na upungufu na uchafu haigongani na nukuu sahihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini wakanushaji wamedai kuwa maandiko ya sifa yanapingana na akili na ndio maana wakayapindisha maana.
Akili kwa ujumla hukubaliana na maandiko kwa kiwango cha yale inayoweza kuyafahamu. Kuna mambo ambayo akili haiwezi kuyafahamu, kama mfano wa zile neema zilizomo Peponi. Akili haiwezi kuyajua kabisa. Mfano mwingine ni yale yaliyomo Motoni. Haya ni mambo ya ghaibu ambayo akili haiwezi kuyafikia. Wale vigogo wakubwa katika hawa wanafalsafa na wasomi wa elimu ya theolojia wao wenyewe wanakubali kuwa kuna mambo ambayo akili haiwezi kuyafikia wala kuyazunguka, jambo ambalo ni hoja dhidi yao. Ikiwa akili inashindwa kufikia maana ya maandiko kwa kina, basi hairejelewi, bali katika jambo hili hurejewa yale yaliyokuja nayo Manabii na kujisalimisha kwake. Wala tusiingie katika mazege ambayo hatuwezi kutoka ndani yake. Hii ndiyo njia ya salama.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 229-230
- Imechapishwa: 15/07/2026
Jambo la nne unaoonesha ubatili wa ´Aqiydah ya wanaokanusha sifa ni kubainisha kwamba akili timamu iliyosalimika kutokana na upungufu na uchafu haigongani na nukuu sahihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini wakanushaji wamedai kuwa maandiko ya sifa yanapingana na akili na ndio maana wakayapindisha maana.
Akili kwa ujumla hukubaliana na maandiko kwa kiwango cha yale inayoweza kuyafahamu. Kuna mambo ambayo akili haiwezi kuyafahamu, kama mfano wa zile neema zilizomo Peponi. Akili haiwezi kuyajua kabisa. Mfano mwingine ni yale yaliyomo Motoni. Haya ni mambo ya ghaibu ambayo akili haiwezi kuyafikia. Wale vigogo wakubwa katika hawa wanafalsafa na wasomi wa elimu ya theolojia wao wenyewe wanakubali kuwa kuna mambo ambayo akili haiwezi kuyafikia wala kuyazunguka, jambo ambalo ni hoja dhidi yao. Ikiwa akili inashindwa kufikia maana ya maandiko kwa kina, basi hairejelewi, bali katika jambo hili hurejewa yale yaliyokuja nayo Manabii na kujisalimisha kwake. Wala tusiingie katika mazege ambayo hatuwezi kutoka ndani yake. Hii ndiyo njia ya salama.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 229-230
Imechapishwa: 15/07/2026
https://firqatunnajia.com/140-ndio-maana-akili-haiwezi-kuwa-marejeo/