Jambo la tatu katika mambo yanayobatilisha ´Aqiydah yao ni kwamba sisi tunajua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja na mambo haya, nayo ni kuthibitisha majina na sifa. Muda wa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja navyo, basi ni wajibu kuvisadikisha na kumfuata. Hivyo asiyevithibitisha anakuwa amemkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anayemkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi amekufuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye aliyekuja na mambo haya ya majina na sifa za Allaah. Kwa hiyo ni lazima kuyaamini. Kama vile alivyoleta swalah na wao wanaswali na wanamsadikisha, basi kwa nini hawasadiki majina ya Allaah na sifa Zake ilihali mambo yote mawili yameletwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Ikiwa mnakataa majina na sifa za Allaah, basi kataneni pia swalah, zakaah, swawm na Hijjah na Shari´ah yote. Ama kuthibitisha jambo fulani na kukataa jambo jingine muhimu zaidi kuliko hilo, basi huu ni upotovu. Kwa hiyo wajibu ni kukubali kila alichokuja nacho Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vinginevyo mtu atakuwa katika wale wanaoamini baadhi ya Kitabu na kukufuru baadhi nyingine. Bali kuamini majina na sifa za Allaah ni muhimu zaidi kuliko kuamini hukumu za matendo, kwa sababu majina na sifa za Allaah ni katika ´Aqiydah.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 227-228
- Imechapishwa: 15/07/2026
Jambo la tatu katika mambo yanayobatilisha ´Aqiydah yao ni kwamba sisi tunajua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja na mambo haya, nayo ni kuthibitisha majina na sifa. Muda wa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja navyo, basi ni wajibu kuvisadikisha na kumfuata. Hivyo asiyevithibitisha anakuwa amemkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anayemkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi amekufuru. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye aliyekuja na mambo haya ya majina na sifa za Allaah. Kwa hiyo ni lazima kuyaamini. Kama vile alivyoleta swalah na wao wanaswali na wanamsadikisha, basi kwa nini hawasadiki majina ya Allaah na sifa Zake ilihali mambo yote mawili yameletwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Ikiwa mnakataa majina na sifa za Allaah, basi kataneni pia swalah, zakaah, swawm na Hijjah na Shari´ah yote. Ama kuthibitisha jambo fulani na kukataa jambo jingine muhimu zaidi kuliko hilo, basi huu ni upotovu. Kwa hiyo wajibu ni kukubali kila alichokuja nacho Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vinginevyo mtu atakuwa katika wale wanaoamini baadhi ya Kitabu na kukufuru baadhi nyingine. Bali kuamini majina na sifa za Allaah ni muhimu zaidi kuliko kuamini hukumu za matendo, kwa sababu majina na sifa za Allaah ni katika ´Aqiydah.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 227-228
Imechapishwa: 15/07/2026
https://firqatunnajia.com/139-ni-lazima-kuamini-na-kusadiki-yote/