Swali: Umesema kitambo ya kwamba kujitibu kwa damu ni haramu kwa mtazamo wa dini. Hata hivyo baadhi wanasema kuwa ni dharurah kwenda kwa kabila fulani na kwamba Allaah (Ta´ala) amesema:
فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ
”Lakini aliyefikwa na dharura pasi na kutamani wala kupindukia mpaka, basi si dhambi juu yake.” (02:173)
Unasemaje juu ya hilo?
Jibu: Kama tulivosema ni haramu na haramu inafaa wakati wa dharurah. Lakini dharurah ni ipi? Dharurah maana yake ni kwamba tujue kuwa mtu akifanya jambo fulani basi inaondoka dharurah yake. Aidha tujue pia kwamba dharurah yake haiwezi kuondoka isipokuwa kwa kufanya jambo hilo. Kwa msem msemo mwingine hakuna dharurah inayohalalisha haramu isipokuwa kwa kutimia sharti mbili:
1 – Tujue kwamba dharurah yake haiondoki isipokuwa kwa kufanya haramu hiyo.
2 – Tujue kweli ya kwamba dharurah yake itaondosha haramu hiyo.
Kwa ajili hiyo ikiwa mtu anachelea kifo basi inafaa kwake kula nyamafu kukitimia sharti mbili hizo. Kuhusu watu hawa waliotajwa katika swali hakuna dharurah yoyote inayopelekea kuwajuzishia kufanya haramu hiyo.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/32)
- Imechapishwa: 15/07/2026
Swali: Umesema kitambo ya kwamba kujitibu kwa damu ni haramu kwa mtazamo wa dini. Hata hivyo baadhi wanasema kuwa ni dharurah kwenda kwa kabila fulani na kwamba Allaah (Ta´ala) amesema:
فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَلَا إِثْمَ عَلَيْهِ
”Lakini aliyefikwa na dharura pasi na kutamani wala kupindukia mpaka, basi si dhambi juu yake.” (02:173)
Unasemaje juu ya hilo?
Jibu: Kama tulivosema ni haramu na haramu inafaa wakati wa dharurah. Lakini dharurah ni ipi? Dharurah maana yake ni kwamba tujue kuwa mtu akifanya jambo fulani basi inaondoka dharurah yake. Aidha tujue pia kwamba dharurah yake haiwezi kuondoka isipokuwa kwa kufanya jambo hilo. Kwa msem msemo mwingine hakuna dharurah inayohalalisha haramu isipokuwa kwa kutimia sharti mbili:
1 – Tujue kwamba dharurah yake haiondoki isipokuwa kwa kufanya haramu hiyo.
2 – Tujue kweli ya kwamba dharurah yake itaondosha haramu hiyo.
Kwa ajili hiyo ikiwa mtu anachelea kifo basi inafaa kwake kula nyamafu kukitimia sharti mbili hizo. Kuhusu watu hawa waliotajwa katika swali hakuna dharurah yoyote inayopelekea kuwajuzishia kufanya haramu hiyo.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/32)
Imechapishwa: 15/07/2026
https://firqatunnajia.com/ni-kipi-kinazingatiwa-kuwa-ni-dharurah/