Swali: Je, inafaa kubadilisha nia kutoka katika swalah maalum kwenda katika swalah nyingine maalum?
Jibu: Haijuzu kubadilisha nia kutoka katika swalah maalum kwenda katika swalah nyingine maalum, au kutoka katika swalah isiyogungamana na kwenda katika swalah maalum. Kinachofaa ni kubadilisha nia ya swalah maalum na kwenda katika swalah isiyofungamana.
Mfano wa sura ya kwanzama, bi maana kutoka katika swalah maalum na kwenda katika swalah maalum, ni mswaliji kubadilisha nia kutoka katika Dhuhr na kwenda katika ´Aswr. Katika hali hii inaharibika Dhuhr kwa sababu ameitoka. Pia haifungiki na wala haisihi ´Aswr kwa sababu hakuinuia kuanzia mwanzo wake. Kwa ajili hiyo atalazimika kuzilipa swalah zote mbili.
Mfano wa sura ya pili, bi maana kutoka katika swalah isiyofungamana na kwenda katika swalah maalum, ni mswaliji abadilishe nia kutoka katika swalah ya Sunnah isiyofungamana na kwenda katika swalah ya Raatibah. Kwa msemo mwingine ameingia katika swalah kwa nia ya swalah ya Sunnah isiyofungamana kisha akataka kuibadilisha kwenda katika Raatibah ya Dhuhr. Swalah hii ya Raatibah haisihi kwa sababu hakuinuia kuanzia mwanzo wake.
Mfano wa sura ya tatu, bi maana kutoka katika swalah maalum na kwenda katika swalah isiyofungamana, ni mswaliji anuie Raatibah ya Maghrib kisha akataka kuibadilisha nia kwenda katika Sunnah isiyofungamana. Hili ni sahihi na swalah haibatiliki. Kwa sababu nia ya swalah maalum imebeba nia ya swalah isiyofungamana. Wakati nia ya swalah hiyo maalum inapofutwa, basi kunabaki nia ya swalah isiyofungamana. Hata hivyo halipwi thawabu juu ya ile swalah ya Raatibah kwa sababu aliitoka.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/448-449)
- Imechapishwa: 30/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/448-449)
Imechapishwa: 30/04/2026
https://firqatunnajia.com/kubadilisha-nia-kutoka-swalah-moja-kwenda-swalah-nyingine-ii/