Swali: Je, inafaa kubadilisha nia kutoka katika swalah maalum kwenda katika swalah nyingine maalum?
Jibu: Haijuzu kubadilisha nia kutoka katika swalah maalum kwenda katika swalah nyingine maalum, au kutoka kutoka katika swalah isiyofungamana kwenda katika swalah maalum. Hata hivyo inafaa ikiwa ni kutoka katika swalah maalum kwenda katika swalah isiyofungamana.
Mfano wa sura ya kwanza, bi maana kutoka katika swalah maalum kwenda katika swalah nyingine maalum, ni mswaliji ameanza kuswali ´Aswr na katikati ya swalah akakumbuka kuwa hajaswali Dhuhr na hivyo akanuia kuwa ni Dhuhr, haisihi. Kwa sababu ni lazima swalah maalum nia yake iwe kuanzia mwanzo.
Mfano wa sura ya pili, bi maana kutoka katika swalah isiyofungamana kwenda katika swalah maalum, mswaliji anaswali swalah ya kujitolea isiyofungamana kisha akakumbuka kuwa hajaswali Fajr au Sunnah ya Fajr na hivyo akabadilisha nia yake kwenda katika swalah ya Fajr au Sunnah ya Fajr, sura hii pia haisihi.
Kuhusu kubadilisha kutoka katika swalah maalum kwenda katika swalah isiyofungamana, mtu akaanza swalah kwa njia ya kwamba ni Raatibah ya Fajr na katikati ya swalah akakumbuka kuwa ameshaiswali, hapa anaweza kubadilisha nia yake ya kwanza na kunuia kuswali tu.
Mfano mwingine ni mtu ameanza kuswali swalah ya faradhi peke yake kisha kukakimiwa swalah, akataka kubadilisha nia kutoka katika faradhi kwenda katika swalah ya kujitolea ili aifupishe Rak´ah mbili, katika hali hii inafaa kwa sababu amebadilisha kutoka katika swalah maalum na kwenda katika swalah isiyofungamana. Hivi ndivo ilivyo kanuni: haisihi ikiwa ni kutoka katika swalah maalum kwenda katika swalah nyingine maalum, haisihi pia kubadilisha nia kutoka katika swalah isiyofungamana kwenda katika swalah maalum na inasihi ikiwa ni kubadilisha kutoka katika swalah maalum kwenda katika swalah isiyofungamana.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/448-449)
- Imechapishwa: 30/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/448-449)
Imechapishwa: 30/04/2026
https://firqatunnajia.com/kubadilisha-nia-kutoka-swalah-moja-kwenda-swalah-nyingine/