Swali: Kuhusiana na yale yaliyozoeleka kwa baadhi ya wanawake ambapo baadhi wanawauliza wengine katikati ya swalah na hivyo wanaitikia ndio au hapana kwa kutikisa kichwa. Je, kitendo hichi kinaiharibu swalah?

Jibu: Hapana vibaya. Kuashiria ndani ya swalah ni jambo halina ubaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiashiria kwa mkono wake anaposalimiwa.

Swali: Vipi kwa ambaye amezungumza kwa kusahau?

Jibu: Hapana neno juu yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21576/حكم-الاشارة-باليد-او-الراس-في-الصلاة
  • Imechapishwa: 20/08/2022