Swali: Sherehe nyingi kunaanzwa kusomwa baadhi ya Aayah kutoka katika Qur-aan tukufu. Je, katika kufanya hivo kuna makatazo?

Jibu: Ikiwa sherehe hii ndani yake hakuna maasi wala mambo yenye kwenda kinyume, kuanzwa kwa Qur-aan ni jambo zuri. Ama ikiwa sherehe hii ndani yake kuna mambo yenye kwenda kinyume na maasi haifai kuanza kwa Qur-aan. Kwa sababu huku ni kuitweza Qur-aan na ni kuitumia pasipokuwa mahala pake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam (09) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/09.mp3
  • Imechapishwa: 07/04/2019