Kuanza kufunga Sha´baan inapofika katikati

Swali: Je, inajuzu kufunga baada ya siku ya 15 Sha´baaan mpaka mwisho wake?

Jibu: Kumekuja Hadiyth inayosema Sha´baan ikifika katikati msifunge. Yule anayetaka kheri aanze kabla ya nusu yake. Nusu ikimfikia hakuna neno akaendelea kufunga. Ama kuhusu yule ambaye hakufunga isipokuwa baada ya nusu, kuna Hadiyth inayokataza hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo-jum_ah-15-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 01/05/2015