Kuandika Qur-aan sehemu safi na ikaoshwa na akaitumia mgonjwa

Swali: Katika mji wetu kuna baadhi ya watu wanaandika Qur-aan kwenye ubao kisha wanaiosha, halafu wanamwambia mgonjwa ajipanguse nayo kwenye mwili wake na anaoga nayo. Je, kitendo hichi kinajuzu?

Jibu: Hakuna neno. Hii ni katika Ruqyah, ya kwamba Qur-aan au Adhkaar zikaandikwa sehemu ambayo ni twahara, kama kwenye sahani, ubao na mfano wa hayo, kisha maandishi hayo yanaoshwa na mgonjwa anakunywa maji yake, au mgonjwa akayaoga. Hakuna neno. Hii katika Ruqyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (74) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14131
  • Imechapishwa: 17/11/2014