Kuandika baadhi ya Aayah kisha kujipangusa nazo na kuzinywa

Swali: Je, kuna dalili inayomjuzishia mtu kuandika kitu katika Qur-aan kisha akajipangusa nayo na kuinywa?

Jibu: Hayo yamefanywa na Salaf na wakaita kuwa ni ”matabano”. Wanaandika kwenye sahani, karatasi na zafarini kisha wanajiosha nayo. Yamefanywa na baadhi ya Salaf. Ibn-ul-Qayyim ametaja kutoka kwa Salaf wengi ya kwamba ni kitendo kinachonufaisha kwa idhini ya Allaah. Mtu anaandika baadhi ya Aayah au du´aa kwa zafarini kisha anajiosha nazo na kuzinywa.

Swali: Kwa hiyo ambaye anafanya hivo hakaripiwi?

Jibu: Hapana vibaya. Kwa sababu sio kuitundika, bali ameinywa tu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24518/حكم-كتابة-شيء-من-القران-ومسحه-وشربه
  • Imechapishwa: 30/10/2024