Hirizi wamekatazwa washirikina peke yao?

Swali: Mtu anapowanasihi na kuwakumbusha wale wanaotundika hirizi hizi wanasema kuwa Aayah hizi zimeteremshwa juu ya washirikina katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba wao eti ni waislamu.

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kutundika hirizi basi Allaah asimtimizie mambo yake.”

Allaah amekataza jambo hili. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia ´Imraan:

”Hakika haikuzidishii isipokuwa unyonge.”

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tena:

”Mwenye kutundika hirizi amefanya shirki.”

Hadiyth zinabainisha kuwa mambo hayo yanazigeuza nyoyo kutoka kwa Allaah na badala yake kuwategemea viumbe.

Swali: Aayah ni zenye kuenea zinawakusanya wao na wengineo?

Jibu: Ndio, kulingana na vile ilivyokuja ndani ya Qur-aan na Sunnah. Kuhusu dawa zenye manufaa na sababu zinazokubalika katika Shari´ah hazina ubaya wowote. Sababu hizo ni kama mfano wa mtu anavyokula na kunywa, akavaa kitu chenye joto wakati wa baridi, kuvaa kitu chepesi wakati wa kiangazi na kujipuliza kwa feni.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24520/هل-النهي-عن-التماىم-خاص-بالمشركين
  • Imechapishwa: 30/10/2024