Swali: Imaam Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amenukuu katika ”Zaad-ul-Ma´aad” kutoka kwa Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) kuhusiana na mnyoa masharubu kwamba anatakiwa kuadhibiwa. Je, inahusiana na mwenye kunyoa kwa wembe au kunaingia pia mashine ya kunyolea?

Jibu: Vyote, ni sawa amenyoa kwa wembe au mashine ya kunyolea. Kunyoa masharubu kunaufanya uso kuwa mbaya. Masharubu yanatakiwa kupunguzwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema masharubu yapunguzwe na yakatwe, hakusema yanyolewe. Kunyoa kunaufanya uso kuwa mbaya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 03/07/2024