Kuacha du´aa kati ya sijda mbili kwa makusudi

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mswaliji endapo ataacha du´aa kati ya sujuud mbili kwa makusudi?

Jibu: Sahihi ni kwamba swalah yake inabatilika, kwa sababu ni wajibu kusema hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kufanya hivo pale aliposema:

“Swalini kama mnavyoniona nikiswali.”

Basi ikiwa hakusema:

ربِّ اغفر لي

”Mola nisamehe!”

kati ya sujuud mbili kwa makusudi, hali ya kuwa anajua hukumu, si mjinga, basi swalah yake inabatilika. Ama ikiwa alikuwa mjinga au amesahau, basi hana dhambi yoyote. Lakini ikiwa alikuwa imamu au anayeswali peke yake na amesahau, basi atasujudu sujuud ya kusahau. Lakini ikiwa alikuwa anamfuata imamu, basi hana haja ya kufanya chochote.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25335/حكم-صلاة-من-ترك-الدعاء-بين-السجدتين-عمدا
  • Imechapishwa: 26/02/2025